Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na
majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano
kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema
kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki
halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele
kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.
Kwa
uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi
(jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo
Uamuzi wa Naibu Spika
Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na wengineo, na kupewa adhabu
ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge, Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba
Muongozo/Taarifa mara kwa mara, Hivyo Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao,
na baadae kitendo cha wabunge hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka
nje ya Bunge pamoja na kuwagomea Askari wabunge, kitendo ambacho kidogo kizue
masumbwi live, Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge,
Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na
adhabu iliotolewa.
Taswira ya vurugu
zilizotokea bungeni dodoma jana ambapo Mbunge wa mbeya Mh mbilinyi akiskiwa
pamoja na wenje, lema na wengineo wakionekana kwa pamoja wakiwazuaia askari ili
wasimtoe nje mh Tundu lissu aliyeamriwa na naibu spika atolewe nje ya ukumbi wa
bunge
hapa waziri wa nchi na uratibu wa bunge Mh William Lukuvi akiwaeleza jambo wabunge wa chadema mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa baada ya kutokea vurugu bungeni