Search in This Blog

JB AJITOSA RASMI KWENYE SIASA

Jacob Stephen Mbura ‘JB’. 
MWIGIZAJI ‘namba wani’ Bongo mwenye heshima kubwa, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ yupo mguu sawa kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kugombea ubunge mwaka 2015.Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda muafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii,” alisema JB.
Hata hivyo, ‘mheshimiwa’ huyo hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea akisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja kubwa lenye upinzani mzito kila ukifika wakati wa uchaguzi.
“Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi,” alisema JB

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger