Search in This Blog

MAKINDA ABARIKI ADHABU KWA WABUNGE



Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania, Anne Makinda hivi punde amesema wabunge watano wa Chadema waliotolewa nje ya Ukumbi wa Bunge na kupewa adhabu ya kukaa nje siku tano ni halali na kwamba itawekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu.

Makinda masema adhabu hiyo ni halali kwa kuwa wabunge watano wa Chadema walishindwa kutii amri  ya Naibu Spika, Job Ndugai ambaye aliwataka wabunge hao watoke nje baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kugoma kutoka nje ya ukumbi.

Katika ukumbi wa Bunge juzi Tundu Lissu alisimama na kuomba mwongozo wa Naibu Spika Ndugai wakati Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alipopewa nafasi ya kuzungumza.

Awali Tundu Lissu aliomba mwongozo lakini Naibu Spika Ndugai alimwambie akae chini na wakati spika huyo akisisitiza akae, mbunge huyo wa Singida Mashariki aligoma.

Baada ya Lissu kutaa Naibu Spika Ndugai aliwaita askari wamtoe nje na hapo wabunge wa Chadema wakiwamo Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi  (Mbeya Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini), Hezekiah Wenje (Nyamagana), Peter Msigwa (Iringa Mjini) walionekana wakijibizana na askari wakati askari hao wakijaribu kumtoa Lissu nje.

Wakari Spika Anna Makinda akitoa adhabu hiyo hivi punde, amesema kwamba kitendo alichofanya Lissu na wabunge hao ni kuwadhalilisha Watanzania.

“Kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na adhabu waliopewa wabunge hao ni halali na itaingizwa kwenye kumbukumbu kwa ajili ya matumizi ya baadaye,” amesema.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger