Search in This Blog

SOMA KAULI ZA WABUNGE WETU ZILIVYOJAA U-COMEDY,

 

 
Chanzo cha umaskini wa wananchi husika husababishwa na bunge bovu na legelege ambalo kimsingi haliwezi kusimamia serikali.

Kwa sasa bunge letu limekuwa comedy show bila kujali pesa za walipa kodi wanazozitafuna kila siku.

Tangu bunge lianze mheshimiwa spika kwa makusudi amekuwa akiruhusu mijadala isiyokuwa na tija bungeni na wabunge wamekuwa wakitukanana matusi ya nguoni
Wakati leo nasikiliza bunge, Mheshimiwa mmoja alisimama tena kwa kujiamini na kudai kuwa eti umasikini wa tanzania unasababishwa na picha ya nyoka iliyoko katika pesa zetu....

"Tanzania ni nchi masikini kwasababu tumeweka picha ya nyoka kwenye hela zetu".... ni kauli ya Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera leo bungeni.

Kauli aliyoitoa Mheshimiwa Bungeni leo haiingii akilini hata kidogo. Labda pengine kwa sababu ya upeo wangu mdogo wa kuelewa na kufikiri .....

Ni vigumu sana kuwashawishi wananchi na jumuia za kimataifa kuwa umasikini na matatizo yote yanayoikabili shillingi ya Tanzania yanasababishwa na picha za nyoka...

Baadhi ya COMEDY toka bungeni:

-Kianzishwe chuo cha kufundisha wanaume namna ya kuwafundisha namna ya kutongoza wanawake - Mbunge viti maalum Chadema!

-Tanzania ni nchi masikini kwasababu tumeweka picha ya nyoka kwenye hela zetu".. hii ni kauli ya Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera

-Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwazika viongozi wa kitaifa watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza Juni, mwaka huu.
-Bangi ihalalishwe na kua zao la Taifa!

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger