Tofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu hao wamebaini kuwa sababu kubwa
zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya zaidi wanapokosa watoto ni
tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila kitu na msukumo wa familia.
Tofauti na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa
ajili yao binafsi kwa asili ya kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu
inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa za utafiti huo ulioongozwa na Robin
Hadley, wa Chuo Kikuu cha Keele, ukishirikisha wanaume 27 na wanawake
81, ambao hawajapata mtoto, uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa
Taasisi ya British Sociological Association, ya Uingereza.
Waohitaji zaidi watoto
Kwa idadi hiyo waliosema wanahitaji watoto ni wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Nusu ya wanaume walisema kukosa mtoto kunawafanya waonekane tofauti kwenye jamii, huku wanawake wakisema wanahitaji watoto ili waje kuwasaidia baadaye.

Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 38 ya wanaume
walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu
ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa wanaume
wanajisikia vibaya zaidi kukosa watoto kwa sababu asilimia ya wasio na
watoto ni wanaume,tofauti na wanawake ambao wakati mwingine hubahatika
kupata mmoja au wawili.
Tafiti hizo zilionyesha kuwa kati ya kila wanaume
wanne mmoja hana kabisa mtoto ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake
ambao hawana watoto.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa asilimia 56 ya
wanaume hawana watoto kabisa, ikilinganishwa na asilimia 43 ya wanawake
ambao hawana.
Akizungumzia utafiti wake Dk Hadley, anaeleza
kwamba amegundua kuwa kati ya wazazi wawili aliye kwenye hatari ya
kukosa mtoto kabisa ni mwanaume, huku akiumia zaidi anapopatwa na hali
hiyo kiasi cha kuwa na hasira, kujisikia vibaya mbele za watu, kujitenga
na jamii, kuwa na wivu na mambo yanayofanana na hayo.
Wanawake kupenda watoto
Anabainisha kuwa hiyo ndiyo sababu inayowafanya wanawake wapende kupata watoto kuliko wanaume ili kuwaondoa kwenye matatizo hayo, ambayo mara nyingi husababisha familia nyingi kusambaratika bila kujali zilikuwa kwenye maelewano ya kiasi gani.

Alisema kwamba utafiti huo ulifanyika kwa njia ya
kukusanya maoni kwenye mtandao, midahalo, kujaza dodoso za majibu na
ulihusisha watu wenye umri wa kati ya miaka 20-66 huku wengi waliojibu
maswali hayo walikuwa na umri usiopungua miaka 41.