Search in This Blog

TIZAMA HIZI PICHA ZA TUKIO ZIMA LA HUKUMU YA SHEIKH PONDA NA WENZAKE 49 KUTOKA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.
Akiteta jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.
Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
Msafara ukiwa na ulizi mkali
Akaingia kwenye gari!

Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa gari lake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito lwenye mataa ya Maktaba Squire. 

Wafuasi wakajimwaga barabarani kwa furaha

Wafuasi wa Sheikh Ponda wakilifuata gari wakishangilia
Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.

Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kkusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasiwake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.
Tumewashinda
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda na Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.
Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!
Kama kawaida walikuwepo pia!

HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. ...

Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo. 
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
 
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
 
2.Upande wa Serikali haukuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
 
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
 
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
 
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger