Search in This Blog

WAGOMBEA MAITI KWA WIKI MOJA SASA



 

Mgogoro wa kugombea maiti katika Hospitali Teule ya Lutheran, wilayani Karatu, umechukua sura mpya baada ya ndugu wa pande mbili kuweka walinzi katika mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti, ili kulinda maiti hiyo
Mgogoro huo umedumu kwa takriban wiki moja sasa na umeshindwa kupatiwa ufumbuzi baada ya pande hizo mbili kushindwa kuelewana.

Kitendo hicho kimesababisha mwili wa marehemu kuendelea kuhifadhiwa katika chumba cha maiti.
Wakizungumzia tukio hilo, ndugu wa marehemu Elizabert Mathayo, ambao hadi sasa wako katika mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti, walisema wameamua kufanya hivyo ili kuzuia mwili usipelekwe Lindi kuzikwa na badala yake azikwe katika nyumba yake aliyokuwa akiishi na mume wake
"Nyumba hii ni ya watoto na marehemu alishamzika baba yake hapo, kwa hiyo hatuoni sababu ya ndugu yetu kwenda kuzikwa Lindi wakati ana sehemu ya kuzikwa," alisema dada wa marehemu.
Walisema marehemu ameacha wasia unaotaka azikwe katika eneo alilopewa na baba yake.
Mume wa marehemu, Andrew Saulo alisema yeye ni mume halali na kwa hiyo uwezo wa kumzika mke wake popote anapotaka.
Alisema kwa msingi huo, ameamua kwenda kumzika mke wake Lindi ambako ni nyumbani kwa wazazi wake.
Hadi kufikia jana mchana, mume wa marehemu aliendelea kuwa na msimamo kutaka mkewe akazikwe nyumbani kwake,.
Mume huyo ameweka walinzi nyumbani kwake kuzuia watu wasiingie.
Mkuu wa Wilaya a Karatu, Daudi Ntibenda alisema yeye si msemaji wa jambo hilo ambalo alisema ni la kifamilia.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger