Nayman akimtoka beki wa Mexico
Shabiki wa Brazil
TIMU ya
taifa ya Brazil imeshinda mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara, huku
kijana mdogo mwenye kipaji cha ajabu, Neymar akifunga bao tamu ndani ya
dakika 10 za kwanza kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili
Jo.
Brazil imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
Daniel
Alves alipinda krosi kutoka kulia na nyota mpya wa Barcelona, Neymar
akaitokea wa kwanza mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na
kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande
Jo kufunga la pili.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha
Brazil kilikuwa: Cesar, Alves, Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo,
Paulinho, Oscar/Hernanes dk62, Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred.
Mexico:
Corona, Rodriguez, Salcido, Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno,
Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68