
Siku kadhaa zilizopita baada ya LK4 kurudi nchini kwao Uganda alitweet kuwa kuna ‘Eviction party’ inakuja, na kuongeza kuwa kama mambo yataenda vizuri anategemea kupata mgeni rasmi japo hakumtaja kwa jina na kutuachia uwanja wa kutabiri kuwa ni kipenzi chake Koketso.
Siku zikaenda bila kupata updates zozote kuhusu party hiyo wala mgeni huyo mpaka alhamisi iliyopita (June 20) baada ya Koketso kutweet, “Hello lovelys!!! Flying out won’t be tweeting till tomorrow. Miss you all already;)”, ndio watu wakahisi huenda ndio safari ya yule mgeni ambaye LK4 anamtegemea.
Kesho yake Ijumaa (June 21) LK4 aliweka picha ya yeye na Koketso wakiwa kwenye gari (huenda wakitokea airport baada ya kumpokea mgeni wake aliyewasili Uganda) iliyosindikizwa na tweet hii, “Life in the Emerald house is great and amazing! They say love conquers all, even borders, well, Is it true? Stay tuned.”.

Kutokana na lovebirds hawa kutaka kutwist kidogo akili za followers wao wa twitter, mrembo kutoka South Africa Koketso naye alitweet tena Jumamosi (June 22) “Hello Africa! Oook I’m good but don’t ask where I am. Lol!”
Well, kwasababu wameamua kutoa matukio kwa episodes tutegemee updates mpya kutoka kwa wawili hawa ambao inaonekana wanampango wa kutu surprise, lets wait and see!