NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa
usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi
Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani,
Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwepo ikifanya kazi chini ya uratibu
wa Ijumaa Wikienda.
KWA NINI MTAA UFUMULIWE?
Kwa mujibu wa takwimu za kiserikali, eneo hilo
(kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori) limekubuhu kwa wasichana kujiuza
nyakati za usiku huku makao yao makuu yakiwa eneo la Afrika Sana hasa
pembezoni mwa Corner Bar.
Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa ya eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema:
“Tumejitahidi
sana kushirikiana na polisi ili kutokomeza ukahaba eneo hilo lakini
wapi! Hawa mabinti ni wabishi, mbaya zaidi wamelifanya eneo hili kuwa la
ngono.
“Watoto wetu wanapita usiku pale wanawaona wanavyofanya,
wanatuharibia kizazi kijacho, kama wao wamejishindwa wasiwaambukize
wengine.”
TIMU ILIYOENDESHA OPERESHENI
Siku ya tukio, saa tisa usiku, askari wa ulinzi shirikishi walijipanga
kwa ajili ya kuufumua mtaa huo huku wakiwa na tahadhari kufuatia habari
za kiintelijensia kudai kuwa, makahaba hao walipanga kuua mtu punde
watakapovamiwa.
Askari hao wakiwa kwenye doria ya kila usiku,
waliwavamia makahaba hao eneo lenye majani madogo katikati ya Afrika
Sana na Mapambano upande wa yadi ya Mwanamboka wakiwa na wateja wao
wakifanya ngono hadharani.
NUSURA DAMU IMWAGIKE
Katika hali iliyoonesha makahaba wamejiimarisha kwa ulinzi siku hizi,
wakati wa zoezi hilo, machangu hao sanjari na vibaka wanaowaunga mkono
wakisemekana ni ‘walinzi’ wao, waliokota mawe na kuwarushia askari hao
hali iliyozua tafrani zaidi.
Ndipo piga nikupige ilipozuka ambapo
askari walionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kwa kuwadhibiti
kwa vichapo vya hapa na pale na kufanikiwa kuwaweka wengi chini ya
ulinzi.
Kuona hivyo, baadhi ya makahaba na wateja wao walifanikiwa
kuwachoropoka askari bila nguo na kutokomea gizani hivyo kulifanya eneo
hilo kuwa jeupe.
WENGINE WAKIMBIA NA KUACHA NGUO ZA NDANI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya makahaba waliokimbia
walijikuta wakiacha kwenye majani nguo zao za ndani na kuzua maswali
kwamba ni kwa nini hawakuwa wamezivaa!
“Jamani hizi si nguo zao za
ndani? Ina maana wakiwa kazini hawavai siyo? Wanakuwa tayaritayari kwa
kazi? Jamani!” alisema kwa mshangao mkubwa mmoja wa askari hao.
MAKAHABA WALIONASWA WALONGA
Licha ya kuwa chini ya ulinzi mkali, baadhi ya makahaba walionaswa
walikuwa wakiwalalamikia askari hao kwamba wanawafuatafuata wakati kila
mtu siku hizi anaangalia atakulaje!
“Mnatuonea bure, nyie mnakula
kivyenu na sisi mngetuacha tule kivyetu, hao watoto wenu mnaosema
tunawaharibu usiku huu wao wanatokea wapi na wanakwenda wapi?” alisikika
akisema kahaba mmoja aliyekuwa mtata kuwekwa chini ya ulinzi.
Mwingine akadakia: Kama mnataka tuwape uroda si mseme, mnatukamata kila
siku kwani tunawatibulia nini majumbani mwenu? Lini tumekuja kuwaghasi
wakati mmelala na wake zenu?”
Uchunguzi wa kawaida ulibaini kuwa
muda rasmi wa makahaba hao kuwasili eneo la Corner Bar ili kuanza ‘kazi’
ni saa mbili usiku japokuwa wapo wanaoripoti mapema na kufanya biashara
hiyo kwa wizi kulingana na wateja wenye ‘kiu’ nyakati hizo.
AHADI YA MAKAHABA
Licha ya kuwa chini ya ulinzi, makahaba hao waliahidi endapo
watapelekwa polisi na kutoka watarejea eneo hilo kujiuza kwani ndiyo
ajira inayowafanya waendelee kuishi katika Jiji la Dar es Salaam,
kusomesha watoto vijijini kwao na kuwasaidia wazazi wao mahitaji
mbalimbali.
“Hata kama mtatupeleka polisi, tutarudi tu hapa, sisi
tunasomesha watoto, tunasaidia wazazi wetu vijijini, pia tunaishi Dar
kwa sababu ya kipato hiki cha kuuza miili yetu, acheni hizo,” mmoja wa
makahaba hao alisema bila kumung’unya maneno.
MWENYEJI WA MTAA ANENA
Akizungumza na paparazi wetu eneo la tukio, mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye pia ni askari wa ulinzi shirikishi alisema:
“Kufuatia vitendo hivi kushamiri hapa mtaani hadi kufikia hatua ya
makahaba na wateja wao kufanya ngono hadharani kama wanyama, tuliamua
kukimbilia polisi kutoa taarifa, kwa hiyo tuna baraka za serikali za
kuwatokomeza hawa machangu.”
NDIYO DAWA?
Mapaparazi wa Global Publishers wana uzoefu na makahaba wa mtaa huo unaoanzia Bamaga hadi Sinza Mori, ni wagumu kubadilika.
Mara kadhaa, OFM imekuwa ikiwafumua makahaba hao lakini siku inayofuata
wanarudi tena na kupiga kambi kama hakuna tukio lililotokea jana yake!
OFM waliondoka eneo la tukio na kuwaacha askari hao na ‘watuhumiwa’ wao
wakisubiri namna ya kufika kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’, Dar kwa hatua zaidi za kisheria.
SORCE: GPL