Search in This Blog

MZEE NELSON MANSELA YUPO MAHUTUTI HOSPITALINI



Madaktari wanao mtibu rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishiribi na nne zilizo pita na sasa ni maututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika kusini.Taarifa hiyo imesema kuwa mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini pretoria kwa siku kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyo sababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amemtembelea mzee mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matibabu wanao mtibia.

Baadaye bwana Zuma alilejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea mzee Mandela apate nafuu. 
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger