Kupitia Clouds E ya Clouds TV jana rapper kutoka Mbeya Quick Rocka
amefunguka juu ya ngoma yake mpya inayokuja tarehe 31 mwezi huu pamoja
na video yake.
Kwenye interview Quick Rocka amesema, “it’s almost a year now tangu
nitoe kazi kwa watu wangu. Sasa hivi nimekuja na kitu kinaitwa my baby
ndani yake yupo the late CowObama na Shaa. Tarehe 31 mwezi huu ndiyo
nitaiachia ngoma na video yake pamoja. My plans ni kufanya launching
kwenye kiota kimoja wapo cha starehe na ofcoz utaiona trailer/teaser ya
video yenyewe hapahapa kupitia Clouds E.
VIDEO:
Kuhusu sehemu ya Mangwair kwenye video hiyo, Quick amesema: “Sehemu
ya Mangwair verse yake itakuwepo kama kawaida, kuna replacement nzuri
ambayo tunaamini watu wataipenda tumeifanya hapo. So, what is it na nini
tutafanya let it be suprise video ikitoka.”
Clouds E (all entertainment news) huoneshwa kila siku saa mbili usiku kupitia Clouds TV