Search in This Blog

'' WANAWAKE WATEJA WETU WAKUBWA'', WAGANGA WA KIENYEJI WASEMA


b1 ee40f
Kuna aina nyingi za limbwata, kuna kaligoligo, shuntama (Maana kwa kiswahili inama) ya Kanda ya Ziwa ambayo akipewa mume, kila atakachoambiwa na mke atafanya. Lakini kuna limbwata ya kisaikolojia ambayo ni huduma bora na maalumu kwa mume, hii mara nyingi hupatikana maeneo ya mwambao.
Vibao vya matangazo vilivyozagaa nchini vikitangaza huduma kutoka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji, havidanganyi. Vinadhihirisha ukweli kuwa wapo wateja wanaohitaji huduma hiyo kwa wingi.
Aina za dawa
Mfano dawa za kumlinda mume ziko za aina mbili, zinazofanya kazi ya kumkosesha nguvu ya kufanya tendo la kujamiiana anapokwenda kwa hawara na zile ambazo humfanya moyo uwe mzito kusaliti ndoa.
Uchunguzi wa gazeti hili katika viunga vya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa katika kila vibao kumi vya matangazo, vinane vilitaja huduma ya kumtuliza mpenzi, mume au mke.
Ilibainika kuwa waganga wengi wa kienyeji, wanatoa dawa za mapenzi kuliko hata zile za kupandisha cheo, kutoa mikosi au za bahati.
Mganga mmoja, kwa jina la Bibi Maajabu, alisema wateja wake wengi ni wanawake ambao hufika kumwona kwa ajili ya kupata dawa za kumdhibiti mume.
“Wengi wanafika hapa wanaomba dawa za kumdhibiti mume, wanaume wanaokuja kwa ajili ya kuwadhibiti wake zao si wengi kama walivyo wanawake,” alisema Bibi Maajabu ambaye anapatikana maeneo ya Njia Panda ya Kigogo.
Alisema yeye anatoa dawa kwa wanawake hao, dawa ambazo hata hivyo anadai ni siri yake na wateja wake tu.
Bibi huyo alisema dawa zake zinafanya kazi kweli na wala hakuna utapeli kama wafanyavyo waganga wengine.
Mganga mwingine, mkazi wa Tandale maarufu kwa jina la K, yeye hakutofautiana na Bibi Maajabu. Alisema wateja wake wakubwa ni wanawake hasa wenye matatizo ya ndoa na hufika kwake kutaka kupata ‘mwarobaini’ wa kumdhibiti mume.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger