Search in This Blog

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI:

Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma kichwani.Picha ya X-ray ikionyesha jinsi chuma hicho kilivyoingia kichwani mwa bwana Liu. (Picha: HAP/Quirky China News/Rex)

FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya kuchomwa na chuma kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20.

Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na chuma hicho kilichomchoma kichwani.

Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema: 

"Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la damu."Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.

Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger