Mabinti
wa kazi ni sehemu ya familia zetu kutokana na majukumu ya nyumbani
tunayoawaachia ikiwemo mapishi,malezi ya watoto,uangalizi wa nyumba n.k.
Tunaaswa kila mara kuishi nao vizuri maana nao ni binadamu na
wanahitaji upendo. Si kila mtu analitambua hili,ukatili na unyama kwa
mabinti hao umeendelea kushika kasi kila kukicha!
Binti
mmoja (jina tunalo) kutoka Mtwara aliyeletwa Dar es salaam kuja kufanya
kazi amejikuta kwenye mateso makali baada ya kutelekezwa bila nauli na
kukutana na fataki aliomshawishi na kumuweka kinyumba na kusababisha
majanga
Akizungumza na Hatua Tatu ya Times fm Binti
huyo amesema,Akiwa na umri wa miaka kumi na tano (15) tu, alitolewa
kwao Mtwara na kuletwa hapa Dar na dada mmoja aliyemtaja kwa jina moja
la Sophia kwa ajili ya usaidizi wa kazi za ndani.Kwa maelezo yake
ilitokea siku alimchapa mtoto wa bosi wake ndipo bosi alipokasirika na
kufikia hatua ya kumtimua bila ya kumpa nauli ya kurudia kwao.
Alikutana
na baba mwenye mke na watoto wa nne akamshawishi atampa maisha mazuri,
akamweka kinyumba na kuanza kumtumia kimapenzi kinyume na maumbile.
Kutokana na umri mdogo alionao,ilimsababishia kuharibika sehemu zake za
siri na baba huyo na kumtelekeza baada ya kumtomlipia kodi sehemu
aliyompangia chumba na majirani wa hapo ndio waliomsaidia.
Hivi
sasa binti huyo ameoza sehemu zake za siri anamiminika usaha tu na
amehifadhiwa hospitali ya Amana anakopatiwa matibabu na misaada midogo
kama chakula.Cha kusikitisha zaidi baada ya kupimwa kakutwa na Ujauzito wa miezi mitatu na kapimwa virusi vya UKIMWI ambapo Vipimo vinatoka leo alhamisi kujua kama kaathirika au la.