Diwani wa kata ya nduli,aliyejimilikisha kata yote ya nduli
na wananchi wote na kuwa na hati miliki ya eneo hilo,na hata kuwatuma watoto
wake wa kuzaa mwenyewe wavamie mkutano wa chadema na kuwakatakata mapanga
makamanda wetu wa iringa na kumuachia kilema kamanda wetu oscar mwanachuo wa
ruco(kahitimu mwaka jana) kwa vile tu tulikwenda kutoa elimu ya ukombozi ktk
kata yake.
Na hatimaye sheria
ikachukua mkondo wake na kushtakiwa yeye pamoja na watoto wake waliotuvamia,na
aliyekuwa akitinga mahakamani na uongozi wote wa ccm wilaya-iringa na misare
yao ya kijani huku akionyesha mihirizi hadharani pale mahakamani,na ambaye kesi
yake inatakiwa kusikilizwa tena kesho mahakama ya mkoa-iringa,leo mchana
amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla na kupelekwa hospitali ya mkoa
yalikomkuta mauti,hivyo kuwaachia watoto wake kesi ya kushambulia na kujeruhi
wanachama wa chadema.