
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah
al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika
kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa
kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha
matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana
Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na
hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba
ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa
mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi
mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo
ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya
huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa
kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.