Mama
Sharo ametiririka kuwa kuna Gari aina ya Oper, ambayo alikubaliana na
Mudy Suma rafiki wa Marehemu Sharo kwamba iuzwe halafu yeye wampelekee
Pesa bado hajapewa wala kuambiwa chochote, pia kuna Pesa za Pango la
nyumba aliyokua ameikodisha sharo milionea, kwa sababu sharo alihamia
katika nyumba hiyo na kuishi kwa muda mfupi ndo akafariki dunia,
Nilipomuuliza
kuhusu Bajaj ya iliyooachwa na Sharo, mama alijibu kuwa Bajaj hiyo
inafanya kazi ya kubeba abiria jijini na Pesa za biashara hiyo amekua
akitumiwa karibu kila wiki na kijana aliyekabidhiwa kuiendesha.
Mama
Sharo aliongeza kuwa anaomba wahusika wampe haraka Pesa hizo ili
akajenge nyumba kwenye kiwanja kilichoachwa na marehem maeneo ya Mbezi
kwa sababu akichelewa chelewa watu watakimega kiwanja au kukidhulumu
kabisa.
Licha
ya mali zilizotajwa hapo juu, pia kuna movie aliyoigiza Sharomilionea
na Kitale hajaambiwa imeishia wapi japo bado haijaingia mtaani.
Lawama
zote hizi ameangushiwa Muddy Suma, jamaa ambaye gari yake aina ya
Harrier ndiyo aliyopata nayo ajali Sharomilionea na kusababisha kifo
chake, na walikua wamebadilisha na gari yani Sharo alimwachia Muddy Gari
yake aina Oper, ila Muddy Suma aliahidi atalirudisha gari hilo kwa
wazazi wa Sharo na yeye amesamehe kiroho safi