Kwa
ugunduzi huu hakuna uoga tena wa mgao wa umeme (kwa bongo) ili kuchaji
simu sababu mtu unaweza kuchaji simu yako kwa ‘waste product’ ya mwili
wako mwenyewe.
Wanasayansi wa maabara ya Bristol Robotics Uingereza wamegundua njia
ya kutumia mk*jo kama chanzo cha kuzalisha umeme wa kuchaji betri za
simu, na kudai kuwa wa kwanza kutengeneza “the world’s first microbial
fuel cells (MFC) powered mobile phone”.
Watafiti hao walielezea juu ya ugunduzi wao kupitia jarida la ‘Physical Chemistry Chemical Physics’.
Dr Ioannis Ieropoulos amesema, huo ndio ugunduzi wa kwanza wa
kuzalisha nguvu ya umeme kwa kutumia mk*jo, na katika majaribio ya
utafiti huo wamefanikiwa kuchaji simu ya Samsung. “By harnessing this
power as urine passes through a cascade of MFCs, we have managed to
charge a Samsung mobile phone”. Aliongeza “The concept has been tested
and it works – it’s now for us to develop and refine the process so that
we can develop MFCs to fully charge a battery”.
Wanasayansi hao wanaamini kuwa teknolojia yao inaweza kutumika katika
mabafu huko mbeleni kwaajili ya kuwashia mashine za kunyolea au kupasha
moto maji ya kuoga na kuwasha taa.