Mtanzania mwenzetu Ndg. Shabani Japhari, ambaye amefariki tarehe 1
mwezi huu, kwa kujinyonga mjini Saint Petersburg, nchini Urusi,
anatarajiwa kuzikwa nchini humo Juma hili. Kwa mujibu wa msimamizi wa
mazishi hayo, Ndg. Moses Mango, utaratibu wa mazishi utakuwa kama
ifuatavyo:
1. Marehemu anategemewa kuchukuliwa kutoka nyumba ya maiti Ijumaa tarehe 5 Julai, 2013.
2. Muda wa kuchukua maiti ni saa Sita mchana (12:00 Noon)
3. Kabla ya hapo, kufuatia maagizo ya watu wa nyumbani, kwa muda
wa saa moja nzima, mwili utaogeshwa, kuvalishwa na kuandaliwa kwa
kuzikwa na Imam, akisaidiwa na Waislam wengine wawili. Pia Mango
aliongeza kwa kusema, “Kwa upande wetu, matayarisho hayo ya kiislam
yatawakilishwa na Mr. Silana Juma wa TCC, aliyeko hapa kwa kozi fupi”.
4. Anuani ya nyumba ya maiti ni: St. petersburg, kolpino, 12 Pavlovskaya street.
5. Makaburi ni :New Kolpinsky cementry, na kutakuwa na basi la kuwapeleka watu toka nyumba ya kuhifadhia maiti.
6. Kutakuwa na ujumbe toka ubalozini, Moscow.
Masaa machache baadae, Ndg. Mango alituma ujumbe ufuatao kupitia
mtandao wake wa Facebook, ” Early Morning of July 1st, 2013, I lost a
friend, who became a brother to me. I had a honor to be his friend for
the last 22 years. He was a great man in many senses, a supporting
father, a good samatarian and really good man. Tomorrow we are going to
bury him. Please, join us physically or in your prayers. RIP Japhari
Shabani. Your absence will be heavily missed”, alimalizia kusema Ndg.
Mango.
Kwa hakika, baada ya maneno hayo mazito kutoka kwa Mango,
thehabari tunaungana katika maombolezo na wana familia, marafiki, na
Watanzania wengine wote walioguswa na msiba huu kwa njia moja au
nyingine. Pia tunamuombea Ndg. Shabani, aliyetutangualia mbele ya haki,
mapumziko ya amani.
Picha za hapo juu, ni za marehemu Shabani enzi za uhai wake.