NIMETOA MAISHA YANGU YOTE KWA CHAKULA ASEMA JB, HII NDO SABABU ILIYOMFANYA ASEME HIVYO.
JB mwigizaji wa filamu na Balozi wa Oxfam Tanzania.
MWIGIZAJI Nyota katiaka tasnia ya filamu Swahiliwood Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa maisha yake yote ameyatoa kwa watu wenye shida ya chakula baada ya kuwa balozi wa Oxfam katika kampeni inayoitwa Grow akiongea na FC msanii huyo mwigizaji bora kwa mwaka 2012/ 2013 amesema kuwa ndoto yake ni kuwasaidia watoto wasio na chakula.
.
Masoud Ali, Dina Marios, wakiwa na Jacob Stephen kama mabalozi wa Oxfam
JB katika pozi
JB akiwa na wadau wa Oxfam katika picha ya pamoja.
“Kwanza namshukru Mungu kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Oxfam na kupewa kazi ambayo nimekuwa nikiifikiria siku zote jinsi gani naweza kuwasaidia wenye matatizo ya chakula hasa watoto, kuanzia sasa maisha yangu yote nimeyatoa kwenye chakula nitahakikisha hasa watoto wanapata chakula nikiwa kama balozi wa Oxfam,”anasema JB
JB ni mwigizaji pekee ambaye amechaguliwa kutoka kundi la wasanii wa filamu baada ya nafasi hiyo kuachwa na marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa Balozi wa Oxfam, kwa sasa inawezekana JB ndiyo kawa mrithi wake baada ya takribani mwaka mmoja, wadau kuhofia kukosekana mrithi wa marehamu Kanumba