Search in This Blog

UGONJWA WAKATISHA SWAUMU YA HUSNA MAULID

WAKATI Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, mlimbwende aliyewahi kushiriki Miss Tanzania, Husna Maulid amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kufunga kutokana na kuugua ugonjwa wa malaria.
 
Husna Maulid.
Akizungumza na paparazi, Husna alisema amelazimika kukatisha kufunga baada ya kuugua malaria na kumfanya kuendelea  na dozi lakini hali bado haijawa nzuri kwani mwili wake unakosa nguvu.
“Naumia sana kushindwa kuendelea na mfungo kwa sababu ya kuumwa sijui kwa nini malaria inanitesa hivi, lakini nikipona nitalipiza siku ambazo sijafunga kwani mwezi huu ni wa toba na ninamuomba Mungu anitimizie kila ninachokihitaji katika maisha yangu,” alisema Husna.
Hivi karibuni Husna alitundika picha katika mtandao wa Instagram inayomuonesha akiwa mjamzito, alipoulizwa na paparazi wetu juu ya hilo alisema siyo mjamzito.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger