Search in This Blog

BAADA YA KUMTEMA MKE WAKE, MZEE MAJUTO AFIKISHWA BAKWATA NA HUYO ALIYEMWACHA. KITENDAWILI KUTEGULIWA TAREHE 23.

MAJ1
SIKU chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman ‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake, Amani liko mbele kukuhabarisha.
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto, Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.
Akasema akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji: “Kwani huyo Rehema ndiye aliyenioa?”
Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.
MAJ
Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.
Rehema akasema kutokana na malalamiko yake, viongozi wa Bakwata walimpa barua ya kumfikishia Mzee Majuto yenye kichwa cha habari cha WITO. Kusoma zaidi bofya
Mzee Majuto anatakiwa kufika bila kukosa kwenye ofisi hizo, Septemba 23, mwaka huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na mwanamke huyo lizungumzwe.
Juzi, Amani lilimpigia simu Mzee Majuto lakini muda wote iliita bila kupokelewa.
Toleo la gazeti la Amani lililopita, liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; NDOA YA MZEE MAJUTO YAVUNJIKA. Kwenye utetezi wake, mzee huyo alisema alimwacha mwanamke huyo baada ya kugundua hajatulia.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger