Search in This Blog

BATULI ATUPA DONGO AKINA MASOGANGE NA WENZAKE


STAA mwenye sura ya mauzo kunako anga la Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amewatupia dongo wadada waliokuwa na mtindo wa kusafirisafiri nje ya nchi na kuwachana kuwa sasa hivi wamebuma kutokana na msako mkali wa serikali.
Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Batuli alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, ambapo alitumia lugha tata kuwatupia dongo wadada wa mjini ambao walikuwa hawashikiki kwa safari na kutanua kwenye kumbi mbalimbali za starehe.
“Eti wale wadada wanaojirusha kila siku, siku hizi mbona siwaoni? Na wale waliokuwa wanasafiri kila siku nao wamepotea, ha ha haaa Sembee lol,” aliandika Batuli.


CREDIT: GPL
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger