Search in This Blog

KAKOBE AWAPA VIDONGE MANGULA NA TEREZY


ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospal Bible Fellowship, Zacharia Kakobe amewapa vidonge vyao ‘kavukavu’, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Terezya Huvisa kwa kuwaambia kuwa kama wanataka kwenda peponi hawana budi wajitangaze hadharani kuwa wameokoka.
Kiongozi huyo wa kiroho aliyasema hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kusikia kupitia kwenye redio kuwa Mangula aliimbisha pambio (nyimbo maalum za walokole) kwenye msiba wa Askofu Moses Kulola aliyefariki dunia Agosti 29 mwaka huu na kuzikwa Mwanza.
“Nilishangaa sana kusikia mtu mzito kama Philip Mangula akitajwa kuwa aliimbisha pambio kwenye msiba wa Askofu Kulola, niwaambie pamoja na viongozi wengine wote kwamba mtu aliyeokoka akiogopa kujitangaza kwamba ameokoa hawezi kwenda peponi,” alisema Kakobe.
Alifafanua kwamba wokovu una nguvu kuliko siasa, hivyo akawataka viongozi wote wa chama na serikali kuokoka na kujitangaza bila woga.
Akisumulia jinsi alivyookoka, Askofu Kakobe alisema alifanya hivyo mwaka 1973 akiwa anasoma Mkwawa Iringa lakini akaacha baada ya waliookoka kumsusia alipokuwa akiwasalimia kiimani “Bwana Yesu Afiwe” nao kumnyamazia.
“Nilikuja kuokoka tena baada ya miaka saba kupita na hapo nikawa mwokovu moja kwa moja hadi sasa,” alisema.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger