Search in This Blog

KIATU CHA THAMANI YA TSH.168,000 CHAMUANGUSHA LADY JAY GEE JUKWAANI NA KUTEGUKA MGUU

Lady Jaydee akiwa backstage na kiatu chake kilichosabisha ateleze jukwaani
Katika show hiyo Lady Jaydee alinunua kiatu cha rangi ya blue, kirefu aka high heels chenye thamani ya shilingi 168,000. Yes laki moja na elfu sitini na nane kama masikio yetu hayakutudanganya.
Hata hivyo urefu wa kiatu hicho ameutaja kuwa chanzo cha kuteleteza jukwaani kwenye show hiyo na kukaribia kumwangusha.
“Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali zingine, isitoshe sikuanguka bali nilikaribia. Ila poleni kwa mlioumizwa na hicho kitendo…Nitapunguza urefu wa viatu siku nyingine,” aliandika jana kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Ni bahati mbaya tu, kwani hata Mwanza/Kahama/Dodoma vilikuwa virefu kama hivyo hivyo na sikuteguka,” alitweet kufafanua kuhusu uvaaji wa viatu virefu jukwaani
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger