Search in This Blog

MASOGANGE KUSHTAKIWA TENA TANZANIA

WAKATI wasichana wawili wakitanzania waliokuwa wakiendelea kusota lumande nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kuingia kemikali zinazotumika kutengenezea za dawa za kulevya wakiachiwa huru baada ya kulipa faini ya  R30,000 (Sh4.8 milioni), Jeshi la Polisi nchini Tanzania imepanga kuwatia hatiani mara tu baada ya kuwasili nchini. Taarifa za ndani zilizonaswa na zinadai kwamba Agnes Gerald, maarufu Masogange na mwenzake Melissa Edward, wanaandaliwa shtaka la kusafirisha dawa hizo nje ya nchi na kuchafua jina la Tanzania.  
"Hatua hiyo inachukuliwa dhidi yao kwakuwa sheria za Afrika Kusini zinatofautiana na sheria za Tanzania na ndiyo sababu hata  Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alikwenda nchini Afrika Kusini kufuatilia suala lao," kilisema chanzo hicho. Kwa upande wake Nzowa alipoulizwa alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya.

                                                                                                        Masongange
Hata hivyo Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine. Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko akizungumza na Habarimpya.com mjini hapa jana alisema kwamba uchunguzi wa kisayansi uliomalizika jana umeonyesha kwamba watanzania hao hawakubeba dawa za kulevya, bali walibeba kemikali aina ephedrine ambazo pia hutumika kutengenezea dawa mbalimbali zikiwemo dawa za kulevya ambapo wakati mwingine hutumiwa na madaktari wakati wa upasuaji.
Kwa upande wa Melisa Kapteni Paul Ramaloko alisema kwamba Mahakama ilibaini kuwa, hakuwa na kosa baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa alimsindikiza mwenzake katika safari hiyo na kwamba hakuhusika moja kwa moja katika tukio hilo. “Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.

Mahakama  Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg Afrika Kusini iliyokuwa ikiendesha kesi ya Masogange.
Kapteni Ramaloko alifafanua kwamba utetezi wa Melisa ulikubaliwa na Mahakama baada ya kujitetea kwamba walikutana na Agness ndani ya ndege na baada ya kuteremka, Masogange akamwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa. Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye. Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki. Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger