UBALOZI wa Tanzania, nchini Kenya umesema raia wake moja alijeruhiwa
juzi wakati wapiganaji wa Kikundi cha Al Shababu walipoteka jengo la
Westgate mjini Nairobi. Taarifa iliyotumwa na Ubalozi wa Tanzania jana,
ilimtaja raia huyo kuwa ni Vedastus Nsanzugwanko ambaye ni Meneja katika
Taasisi ya Kimataifa ya Child Protection, inayofadhiliwa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni, (UNICEF).
Taarifa hiyo,ilisema Nsanzugwanko amejeruhiwa kwa risasi na
magruneit katika miguu yake yote miwili na amelazwa hospitali ya Aga
Khan.
“Anaendelea kupatiwa matibabu, huku hali yake inaendelea
vizuri, hata hivyo ubalozi unaendelea kufuatilia kwa lengo la kupata
taarifa zaidi endapo kutakuwapo na Watanzania wengine katika tukio hilo,
“Majeruhi huyu bado yuko hospitali na hatujaweza kumpiga picha,” ilisema taarifa hiyo,”ilisema taarifa hiyo.
Katika
hatua nyingine, Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kwa kushirikiana na
Uongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi Kenya (TWA), umeandaa
utaratibu maalumu utakaowezesha Watanzania waishio Kenya kujitokeza kwa
ajili ya kutoa damu.
Wakati huo huo, Umoja wa Mabalozi wa Nchi za
Afrika ulikutana na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la
kuwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa wakuu wa nchi zao. Taarifa
zinasema wajumbe hao walikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kutoa