Search in This Blog

"NI KWELI NIMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA" REHEMA FABIAN



WAKATI msanii Agness Gerald ‘Masogange’ akisubiriwa kutua Dar baada kumaliza msala wake huko Afrika Kusini, skendo ya baadhi ya wasanii Bongo kuhusishwa na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’, lingine limeibuka ambapo Video Queen Rehema Fabian amekiri kukamatwa nchini China kwa ishu hiyo.

Madawa ya kulevya.
Wiki mbili zilizopita kulizagaa habari kutoka kwa marafiki wa karibu wa Rehema ambao walidai kuwa mshiriki huyo wa Miss Kiswahili 2009 alikamatiwa huko Shaghai baada ya kukutwa na mwanaume aliyekuwa na unga.
Baadhi ya Watanzania waishio China walitofautiana ambapo wakati wengine wakidai kuwa alikamatwa na wapo waliosema kukamatwa kwake kulitokana na kupitiliza muda wa kuishi nchini humo tofauti na viza yake inavyoeleza.
Katika kipindi hicho chote,
Mdadisi Mambo blog imekuwa likimsaka ambapo wikiendi iliyopita lilifanikiwa kuchati naye ili kupata ukweli wa ‘niuz’ hizo.
Mdadisi Mambo blog: Mambo vipi Rehema?
Rehema Fabian.
Rehema: Mambo poa tu. Nani mwenzangu?
Mdadisi Mambo blog: Unachati na gazeti la Ijumaa Wikienda. Kuna taarifa zimezagaa Bongo kuwa umekamatwa na unga China. Hizi habari zina ukweli?
Rehema: Ni kweli nilikuwa mahabusu. Mateso ya huko wee acha tu. Nilipata kesi lakini si yangu ila namshukuru Mungu nimetoka salama.
Mdadisi Mambo blog: Kesi inahusu nini na kama ilikuwa haikuhusu kwa nini ulikamatwa?
Rehema: Nilikamatwa na mtu (hakutaka kumtaja na ni nani kwake) alikuwa na unga, nimekaa mahabusu wiki mbili na siku mbili. Uzuri huyo mtu alikataa mbele ya polisi kuwa hanifahamu na sihusiki ndipo nikaachiwa.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger