
Wakuu wa Tunisia wanasema 
serikali ya nchi inayoongozwa na chama cha Waislamu imekubali kujiuzulu 
katika majuma machache yajayo, baada ya kumalizika mazungumzo na 
upinzani usiokuwa wa kidini.
Serikali ya muda itachukua madaraka na kutayarisha uchaguzi mwengine.Mazungumzo kuhusu namna ya kuunda serikali mpya yataanza Jumatatu.
Chama kikuu cha wafanyakazi wa Tunisia ndicho kilichopatanisha katika mazungumzo hayo baina ya chama tawala cha Ennahda na upinzani.