Search in This Blog

"TUMEJIPANGA KIUHAKIKA JUU YA UGAIDI" KOVA

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limewatoa hofu wananchi wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo ya mikusanyiko, kufuatia shambulio lililotokea kwenye maduka ya Westgate, yaliyopo jijini Nairobi Kenya, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 65 na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa vibaya.
KOVA
Kamanda Kova
Kamishna wa Kanda hiyo Suleiman Kova amesema tangu kutokea kwa tukio hilo, jeshi hilo limeimarisha ulinzi huku wakiwataka wananchi kutoa taarifa za watu wanaowatilia mashaka (Star TV).
Wakati huo huko Kenya
Majeshi ya Kenya yamechukua udhibiti wa mall hiyo ya Westgate iliyoshambuliwa na wanamgambo wa al-Shabab, na kwa sasa yanafanya operesheni ya mwisho baada ya mateka wote kuokolewa.
Milipuko na milio ya risasi imesikika ndani ya mall hiyo leo asubuhi, saa chache baada ya vikosi vya Kenya kuidhibiti kutoka kwa washambuliaji hao. Takriban watu 62 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa kwenye shambulio hilo la Jumamosi lakini idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kuongezeka. Watu 63 hawajulikani walipo.
Kundi hilo la kigaidi limedai kufanya shambulio kama kisasi dhidi ya operesheni za jeshi la Kenya nchini Somalia.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger