Search in This Blog

WASEMAVYO WANASHERIA KUHUSIANA NA HUKUMU YA KUMWACHIA HURU MASOGANGE


Taarifa ya kuachiwa huru kwa Agnes Gerald aka Masogange na mdogo wake Mellisa Edward imepokelewa kwa mshangao mkubwa na Watanzania wengi.
Agnes-2
Si kwasababu hawawapendi wasichana hao na kwamba wangependa wafie jela, bali ni kitokana na namna ambavyo kesi yao ilivyokuwa ikionekana kubwa na jinsi ilivyokuwa ikitawala vichwa vya habari vya magazeti ya Tanzania.
Kukamatwa na mabegi 6 yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine na yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 si kosa la kawaida. Wengi walikuwa wakiamiani kuwa, maisha ya wasichana hao yameshaharibika na ni ngumu kurudi uraiani mapema.
Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni. Naye Melissa ameonekana hana hatia kwakuwa alidaiwa kumsindikiza tu dada yake aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Pia imeonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali ni kemikali aina ya ephedrine. Walibeba kemikali hizo kwenda kufanyia? Hilo ni swali gumu kulijibu.
Uamuzi wa mahakama hiyo na kubadilika kwa maelezo, haujawashangaza tu Watanzania bali pia Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller aliyelieleza gazeti la Mwananchi kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine. Hata hivyo kemikali hiyo ya Ephedrine ina mfumo wa molecule sawa na madawa ya kama phenylpropanolamine na methamphetamine.
Kwahiyo hata kama alikamatwa na kemikali, bado si kitu cha kawaida kwa msichana tu anayejulikana kuwa ni video vixen kusafirisha bidhaa kama hiyo.
Ili kupata uelewa zaidi kuhusu masuala ya sheria, nimezungumza na Sillas John, mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino ambaye ameeleza jinsi kesi za dawa za kulevya zilivyo.
“Huwa inategemea na sheria ya nchi hiyo inasema nini, maana mahakama yenyewe inaongozwa tu na sheria inasema nini,” anasema Sillas.
“Kama kwenye kifungu cha sheria ya Afrika Kusini inasema kwamba mtu yeyote akikamatwa na madawa ya kulevya, haijalishi kiasi gani, atafungwa miaka sita au faini ya milioni 4, basi mahakama haina choice hata kama ingekuwa ni madawa ya kulevya ya trillion 10. Kwasababu kisheria, ukisoma hata katiba yetu ya Tanzania ibara kama ya 13, inasema kwamba mtu yeyote hatapata adhabu ya kosa ambalo amelitenda kipindi ambach hilo kosa halikuwa ni kosa kisheria.
Kwahiyo sheria zimetungwa miaka ile ambapo milioni 4 ilikuwa ni hela kubwa. Katika hali ya kawaida watu wako too emotional ila hawajui upande mwingine wa sheria.”
Sillas amesema hata Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa ambaye ameshangazwa na adhabu ndogo iliyotolewa kwa wasichana hao licha ya kukamatwa na mzigo wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, haijui vizuri sheria.
“Hiyo hukumu imetolewa kwa mujibu wa sheria,” anasema Sillas. Ni ninyi wananchi mnatuchagulia bunge ambalo linatutungia sisi mahakama sheria za kuapply. Leo, any traffic offence Tanzania unaweza ukagonga mtu na akavunjika miguu ukalipa shilingi elfu 20.
Tatizo linakuja kwamba watu wanaona athari za madawa ya kulevya lakini hawalishawishi bunge lao kubadilisha sheria, sasa unategemea mahakama itafanyaje? Kwa sababu kweli haiingii akilini kutoa adhabu ya milioni 4 wakati kosa ni la bilioni 6, milioni 4 ni nini? Lakini ni kwa mujibu wa sheria. Hatoshtakiwa mtu kwa kosa ambalo halijaandikwa kisheria na hatuwezi kutoa adhabu kwa mtu yeyote kwasababu tu amefanya kosa ambalo sasa hivi linaonekana kubwa.
Maana ya jinai kisheria, ni kile kitu ambapo sheria inasema hii ni jinai. Na maana ya adhabu kisheria sio wananchi wanasemaje, ni ile sheria inaposema kwamba ‘adhabu ya kosa hili ni hii’. Makahaka haiwezi kujitungia sheria, haina mamlaka hayo.”
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger