Search in This Blog

WATAMBUE MATAPELI WA MITANDAO NA NJIA WANAZOTUMIA

WAKATI kukiwa na utapeli mwingi katika mitandao ya kijamii sehemu mbalimbali duniani, Bara la Afrika imelezwa kuwa kinara wa utapeli huo kwenye mitandao hiyo ya kijamii.
Geofrey Hilmary  ni kati ya wadau wakubwa wa mitandao ya kijamii aliyeamua kuanika sura za wadada hawa akidai kwamba ni kati ya sura hatari kwa utapeli, Watu mbalimbali hususan watu maarufu ndani na nje ya nchi wamewahi kukumbwa na utapeli wa aina hiyo,matapeli wengi hutumia picha za uongo huku wengine wakitumia picha za wasichana warembo.

Mbali na picha hizi zilizowekwa kwenye mtandao wa Facebook na Geofrey Hilmary kuwa zinatumika kwa utapeli, Habarimpya.com pia iliwai kufanya utafiti na kubaini aina ya utapeli pamoja na nchi wanazotoka baadhi ya mapeli hao, Utafiti huo ulibaini mambo mbalimbali pamoja na njia wanazotumia mtapeli hao wa mitandaoni  matapeli wengi hutoka katika nchi za Senegal na Nigeria,Kenya na Tanzania, matapeli wengi kutoka Senegal wanatumia njia za kuomba akaunti ya benki ili wakutumie pesa.
Katika maelezo yao hupenda kutumia majina na picha za wasichana warembo huku wakidai kwamba wao ni yatima na wanalelewa katika vituo vya watoto yatima baada ya wazazi wao kuuawa katika mapigano na vurugu za kisiasa.

Katika maelezo yao matapeli hao humtaka mtapeliwa kutuma tarifa zake zote kuanzia majina yake matatu kazi yake mtaa anaotokana na namba ya nyumba pamoja na namba ya akaunti ya benki huku wakidai kwamba wazazi wao walikufa na kuacha pesa nyingi benki lakini kutokana na kwamba wao ni yatima hawaruhusiwi kufuatilia pesa hizo.
Wanakwenda mbali zaidi na kumtamanisha mtapeliwa kwamba akisha tuma taarifa zake pesa hizo zitahamishwa kutoka kwenye akaunti ya wazazi wake na kuingia kwenye akaunti ya mtapeliwa na kisha mtapeliwa atashugulikia paspoti na viza ya mtapeli huyo kisha wataambatana pamoja katika maisha ya raha mstarehe.

Njia ya pili ya utapeli wa kwenye mitandao ni ile inayotumiwa na Wanigeria, wanigeria wao wanajia mbili za utapeli moja ikiwa ni kukutaka ununue vitu kama vile magari nyumba ama kukutafutia nafasi ya kazi katika nchi za ulaya, ikiwa sababa na kukutafutia visa ya kwenda kuishi katika nchi hizo.
Nchini Kenya matapeli wengi wa mitandao wanatumia nafasi ya kumdanganya mtapeliwa kwamba watamtafutia nafasi za masomo nje ya nchi hivyo unachotakiwa kufanya ni kujaza fomu maalum wanayokutumia na kwamba utalipia fomu hiyo kati ya dola za kimarekani 100 hadi 150 lakini gharama zingine  za masomo watalipa wao na baada ya hapo watakusaidia kupata kazi katika nchi za Ulaya na Marekani, kisha wataanza kukata asilimia 10 kwenye mshahara wako kwa miaka mitano.
Endelea kuwa nasi, kesho tutakuletea njia za utapeli zinazotumiwa na watanzania, kwani hili la watanzania ni bab kubwa kuliko vyote na ndiyo njia inayowanasa watu wengi hususan wakina dada
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger