Standard Media wametoa taarifa
nyingine ambayo inazidi kulipa shambulio la Westgate nguvu ya kuendelea
kumiliki vichwa vya habari baada ya kuripoti kwamba Magaidi waliofanya
hilo shambulio Nairobi mwezi September walitumia helikopta ambayo
inamilikiwa na mwanasiasa maarufu wa zamani nchini Kenya ambae taarifa
hii haijamtaja.
Imefahamika, sita kati ya magaidi
walitumia helikopta hiyo kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab
mpaka Nairobi kwa kuhofia kushtukiwa mapema na kukamatwa iwapo
wangetumia usafiri wa ardhini.
Wapelelezi wamesema wanaamini kwenye
helikopta hiyo, magaidi hawa walibeba baadhi ya silaha za kivita ambazo
zilitumika kwenye shambulio hili ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya
watu 60 akiwemo ndugu wa Rais Uhuru Kenyatta.
Magaidi hawa wanaaminika kuingia
kwenye kambi ya Dadaab wakitokea Somalia miezi sita iliyopita ambapo
walijifanya Wakimbizi huku wakiendelea kupanga shambulio la September 21
ambapo baadae walichukua hiyo helikopta ambayo tayari Pilot wake
alikamatwa na kuhojiwa na kisha baadae kuachiwa.
Hata hivyo imegundulika pia ndani ya
jumba la Westgate ambalo ndani yake lina maduka na migahawa mbalimbali,
kwenye floor ya kwanza kulikua na raia wa Uturuki ambae alikodi chumba
cha duka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuanza kukitumia kwa biashara
ya kuuza simu miezi sita iliyopita na pia chumba hichohicho kutumika na
magaidi kama sehemu ya kuhifadhia silaha.
Raia huyu wa Uturuki alisafiri kwenda
nje ya Kenya siku moja kabla ya shambulio la Westgate na Polisi
wanaendelea na msako ambao pia unalihusisha gari aina ya BMW ambalo
lilimilikiwa na yeye na kutumika kubeba Magaidi hawa kwenye mizunguko
mbalimbali ya Nairobi.
Kwa kumalizia post hii, kingine cha
kukwambia ni kuhusu Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Wanjiru
kutoka kijiji cha Kangari huko Nyeri kugundulika kwua mmoja wa Magaidi
na mpaka sasa Watu wa usalama wanandelea kufatilia kama na yeye aliuwawa
kwenye majibizano ya risasi kati ya magaidi na vikosi vya usalama.