Search in This Blog

JULIUS NYAISANGAH 'UNCLE J' AFARIKI DUNIA

Marehemu Julius Nyaisangah (katikati) akiwa katika pozi na Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho (kushoto) na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Uwazi Elvan Stambul (kulia) walipokuwa katika semina ya wanahabari Bagamoyo mwaka 2011.
HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Meneja Mkuu wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!  Taarifa zaidi zitawajia baadaye.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger