MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta
akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss
Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali
iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.
Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye
msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini
Dar es Salaam.
KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga
msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na
kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari
iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu
katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel,
Dar.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali,
Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti
kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.
Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji
wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu
(alikula sahani tatu).
TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani
hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati
akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu
aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.
MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa
wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell
with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi
kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).
WAOMBOLEZAJI SASA
Mamia ya waombolezaji
waliokuwepo eneo la msiba huo walionesha kushangazwa na kitendo cha
binti huyo aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza kwake.
Baadhi yao walidai hali hiyo haikuwa ya kawaida na huenda alikuwa ‘amepata kiburudisho’ (alikunywa pombe).
“Sasa binti si uende ndani ukakae? Hapa ni msibani halafu wewe unasema
maneno kama hayo, huoni kama unasumbua akili za wenzako?” mzee mmoja
alisikika akisema wakati Lulu anaondoka.
“Unajua hawa mastaa wa Bongo mimi nimeshawajua kwani nawafuatilia
sana, wakiandikwa kwa mazuri meno thelathini na mbili nje, wakiandikwa
kwa mabaya timbwili kama hili.
“Hiyo habari anayoilalamikia mimi niliiona kwenye gazeti tena ilikuwa
na picha sasa alichokereka ni nini, si kweli au?” alisikika
mwombolezaji mwingine.
Mwombolezaji mwingine alisema Lulu anaweza kuwa na hoja lakini
inakufa kwa vile kama habari ilimkera alipaswa kumtafuta paparazi huyo
kwa wakati wake au afike Ofisi za Global badala ya kujianika hadharani
huku akidai siku hizi amebadilika.
KWA NINI ALIKEREKA?
Habari zilizopatikana
baadaye zilisema kuwa, Lulu alihamaki kumwona mwandishi huyo aliyeandika
habari zake hizo za kula sahani tatu, kwani tangu kutoka kwa stori hiyo
amekuwa akitaniwa na mastaa wenzake wakimwambia ‘yeye ni mbaya sana
kwenye mechi za ugenini’.
Tafsiri hiyo ni kwamba, Lulu amekuwa akila kupitia kiasi kwenye ‘minuso’ (minuso ni vyakula vya bure kwenye shughuli).
AJITENGA NA BONGO MOVIE
Wakati huohuo, Imelda
Mtema anaripoti kuwa, baada ya kufika ndani ya nyumba ya akina Wema,
Lulu alionekana kutotaka kujihusisha na baadhi ya wasanii wenzake wa
Klabu ya Bongo Movie Unity ambapo alijitenga.
Lulu alijitenga kwa kukaa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo ambao hawakupata nafasi ya kupiga
stori na Lulu kama zamani ni Jacqueline Wolper, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’,
Jennifer Kyaka ‘Odama’, Rachel Haule, Kajala Masanja na Eshe Buheti.
Baadhi ya waombolezaji waliokuwemo walinong’ona kuhusu kitendo cha staa huyo kujitenga wakidai kweli sasa amekua.
“Mh! Lulu sasa amekua jamani, naona hataki kabisa ushoga na watu,
alipofika akasalimia na kwenda kukaa na wazazi wake, ni maajabu,”
alisikika akisema mmoja wa waombolezaji ambaye jina lake halikufahamika.
Mwombolezaji mwingine alisikika akisema kuwa mabadiliko yote yanayoonekana kwa Lulu kwa sasa ni kazi ya mama Kanumba.
TUJIKUMBUSHE
Mzee Isaac Sepetu alifariki dunia Oktoba 28, 2013 katika Hospitali ya TMJ, Dar alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya kisukari.
MAZISHI YA MZEE SEPETU
Mwili wa marehemu
ulitarajiwa kuzikwa jana saa kumi jioni Mjini Zanzibar baada ya
kusafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam alikofia.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.