Search in This Blog

MECHI YA WATANI WA JADI YAMSABABISHIA MAUMIVU CHAZ BABA

KIONGOZI na mwanamuziki wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amevamiwa na vibaka na kuporwa simu, fedha na vitu vingine vilivyokuwa mfukoni mwake.
 
Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
Tukio hilo lilitokea juzi Jumapili nje ya Uwanja wa Taifa, Temeke, Dar muda mfupi baada ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga kumalizika.
“Walikuwa wengi, walinizunguka ghafla na kuniibia, lakini nilifanikiwa kumkamata mmoja na kumpiga lakini wenzake waka mwokoa. Japo hawa watoto wa Temeke wanajifanya wajanja, lakini pia nimewa-komesha,” Chaz baba alimwambia mwandishi wetu.
Vibaka hao walifanikisha zoezi hilo kwa kutumia mwanya wa uwingi wa watu waliokuwa wakitoka uwanjani siku hiyo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger