Search in This Blog

MUME AMCHIMBA BITI JACK WA CHUZ

MUME wa staa wa sinema za Kibongo, Gadner Dibibi amemchimba biti mkewe mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ kwenda kujirusha na mashosti zake bila kuongozana naye.
Akipiga stori na paparazi wetu, Jack alisema mumewe hamzuii kwenda kujirusha viwanja lakini anachotaka ni kuona wanaambatana kama kumbikumbi kitu ambacho kinamweka njia panda kwani marafiki zake huwa wanashindwa kujiachia pindi wanapokuwa na mumewe huyo.
“Mume wangu amenizuia kabisa nisitoke peke yangu na hata mashosti zangu wakihitaji kampani yangu hulazimika kunifata kiwanja nilichopo na mume wangu, sina ujanja tena nishaolewa miye,” alisema Jack.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger