Search in This Blog

SOMA UCHEKE UJUMBE HUU WA FREEMASON BAADA YA JAMAA KUKOSEA KUTUMA HELA KWA M PESA

Jamaa mmoja si akakosea namba na akatuma Shs500,000/-kwa MPESA kwenda namba tofauti na aliyotaka? Hapo hapo akili ya haraka ikamjia akatuma SMS kwa hiyo namba kama ifuatayo. 

MPENDWA TUNATEGEMEA UMEPATA FEDHA ZETU. WEWE NI MMOJA ULIYEBAHATIKA KUUNGANISHWA KATIKA KUNDI LETU TUKUFU LA FREEMASON. ILI KUKAMILISHA MAKUBALIANO NDUGU YAKO WA KARIBU ATAFARIKI KATIKA MUDA WA MASAA MATATU BAADA YA KUPOKEA FEDHA HIZO. MARA HILO LITAKAPOTOKEA FIKA UPESI KWENYE NJIA PANDA YOYOTE ILIYOKARIBU NAWE, NA MTUMISHI WETU ATAKUFUATA NA GARI JEUSI NAWE UTAKUJA KUNYWA DAMU YA KIAPO ILI UWE MWANACHAMA KAMILI.
 
KARIBU KWA FURAHA KUU.........
Dakika moja na nusu baadaye meseji ikarudi kwa jamaa ikisema
“D5RYE289 Imethibitishwa Umepokea Tsh510,000 kutoka kwa ………………………… Tarehe 10/10/13 saa 8:12 AM
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger