Search in This Blog

"TUNABAHATI YA KUZIFUNGA TIMU ZA MAJESHI" ..... GILBERT KAZE AMBAYE NI MCHEZAJI WA SIMBA

 
BEKI wa kimataifa wa Simba, Gilbert Kaze ambaye ni raia wa Burundi amesema wana bahati kubwa ya kuzifunga timu za jeshi tangu msimu huu uanze, hivyo mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utaendeleza rekodi yao ya ushindi mfululizo.
Simba imeshacheza dhidi ya Mgambo, Rhino Rangers, JKT Oljoro na JKT Ruvu ambazo zote ni za jeshi na kufanikiwa kuzifunga huku moja dhidi ya Rhino ikitoa sare. 
Kaze amesema kuwa hawana hofu na Ruvu licha ya kuwa haifahamu lakini rekodi yao katika timu za majeshi walizocheza nazo inaonyesha kuwa wana bahati nazo.
“Tumecheza mechi kadhaa na timu tofauti lakini tunaonekana kama tuna bahati sana kuwafunga wanajeshi, hivyo hatuwaogopi hao tutakaocheza nao Jumamosi, lazima tufanye vizuri.
“Tutahakikisha tunafanya vizuri na kuwafunga wanajeshi, japo kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa sana kwenye mechi,” alisema Kaze.


 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger