Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na
moto.
Mkazi wa kitongoji cha Kijiweni
kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza,
amefariki dunia baada yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki
dunia akiwa ndani ya nyumba yake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Mwenyekiti wa kitingoji hicho Bw. Juma Mashauri, amemtaja aliyekumbwa na mauti
hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36) mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya
Busega Mkoa wa Simiyu.
Bw. Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea
mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo
inaelezwa kuwa ni kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake
na mke wake alitajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha
NGOMA ‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani
Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo
hazieleweki kuwa ni za nani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema
wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana
katika ndoa yao iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vililosababisha mmoja wa
wa wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi ya
kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
Kutokana na tukio hilo kwa upande wake
Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema
Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia
tukio hilo amewaomba vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala
la ulevi unaopelekea kuchukua maamuzi ya kujiua angali taifa bado linawategemea
.
Naye diwani wa kata hiyo ya Chifunfu Robert
Madaha amesikitishwa kwa kutokea kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha
unywaji wa pombe ambao hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.