LICHA ya wenyewe kukanusha kwamba hawajarudiana, ushahidi kwamba
masupastaa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu ni wapenzi
tena umeanikwa, Risasi Jumamosi linao.
Kwa sasa Wema yuko nchini
China akivinjari, lakini habari zisizo na hata chembe ya shaka, zinasema
Diamond naye ametua huko na kuungana na mchumba wake huyo wa zamani.
WAONEKANA MITAANI
Picha za mnato za wawili hao wakiwa kwenye
mitaa mbalimbali jijini Beijing, China zimenaswa na kusambazwa kwenye
mitandao makini hasa baada ya Diamond hivi karibuni kukanusha kupitia
redio moja kwamba hajarudiana na Wema.
Ndani ya picha hizo, Diamond
anambusu Wema kila wakati bila kujali macho ya Wachina ambao kwao hawana
mapenzi ya hadharani kama wazungu.
WAONEKANA CHUMBANI
Picha nyingine zinawaonesha wawili hao wakiwa
chumbani katika mavazi ya kulalia huku wameshika simu kwa ajili ya
kujipiga picha, kama kawa Diamond anambusu mlimbwende huyo huku naye
akionekana kukolea.
USHAHIDI KWA PENNY
Katika Gazeti la Amani la Oktoba 3, 2013 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; Habari ya mjini…WEMA,
DIAMOND WARUDIANA!
Miongoni mwa watu walioongea na gazeti hilo
kuhusu kurudiana kwa wawili hao ni mchumba wa sasa wa Diamond, Penniel
Mungilwa ‘Penny’ ambapo alikiri kusikia Wema na Diamond kurudiana lakini
akasema hawezi kukubali hadi aone picha. Picha ndiyo hizo ukurasa wa
kwanza. Baadhi ya watu wanaotoa maoni yao mtandaoni, wanamcheka!
ANACHODAI DIAMOND
Kwa upande wake Diamond alipoulizwa na
mapaparazi wetu kuhusu kurudiana na Wema na kwamba wapo wote China
wakila bata, alikataa akidai yupo Nigeria kikazi zaidi.
Akadokezwa: Kama upo Nigeria mbona kuna picha unaonekana umepiga ukiwa na Wema?
Akashtuka: He! Hebu n’tumie picha moja niione.
Alipotumiwa picha moja akacheka kidogo kisha akasema: Hii ni filamu bwana. Mimi sijarudiana na huyo demu (Wema).
KUMBUKUMBU MUHIMU
Baada ya kuachana siku za nyuma, Wema na
Diamond waliwahi kudaiwa kwamba wamerudiana na wakahojiwa katika kipindi
cha You Heard cha Redio Clouds FM ambapo wote walikanusha kurudiana.
Halafu Wema akaulizwa: Lakini si bado unampenda Diamond?
Majibu yake: Siwezi kumpenda Diamond wewe.
MASWALI YA MSINGI
Diamond aliwahi kumrekodi Wema akijibembeleza
kwake warudiane, akaipeleka sauti hiyo redioni na ikasikilizwa na raia.
Kwa Wema ule ulikuwa udhalishwaji mkubwa. Je, ni kweli anaweza
kumkubalia msanii huyo washuti filamu pamoja?
Diamond anajua Penny
ameambiwa wao wamerudiana, alipoulizwa na Penny alimjibu achana na
maneno ya watu. Je, Penny anaweza kumruhusu Diamond acheze filamu na
Wema?
Kama ni filamu, Diamond hana vifaa vya kushutia wala kampuni
ya filamu, Wema ana kampuni kubwa yenye vifaa vyote, kwanini
‘makamera-mani’ wake wote wabaki Dar, huko China wamekodi vifaa? Na
kameramani je, pia wamemkodi? Haiingii akilini.
UKWELI UTABAKI PALEPALE
Katika yote, ukweli unabaki palepale
kwamba, wawili hao kwa sasa ni mapenzi motomoto. Chanzo kimoja cha
karibu yao huko China kimeliambia Risasi Jumamosi kwamba, wawili hao
wanatanua kama wako fungate, tena wanalala na kuamka!