Wakenya zaidi ya sitini walipoteza maisha yao katika jumba la Westgate lakini
hadi sasa Wakenya hawajajua ukweli kuhusu yaliyojiri katika jumba la Westgate.- Je ni kweli kuna waliokuwa wametekwa nyara na magaidi na kuzuiliwa katika jumba hilo?
- Je ni kweli kuna magaidi waliouawa na wanajeshi?
Meza ya upekuzi ya Jicho Pevu na Inside Story usiku na mchana wamekuwa wakidurusu kila ukurasa na kufanya mahojiano na kupitia hatua kwa hatua video za CCTV kutoka jumba la Westgate na sasa wako tayari kukusimulia kilichojiri.