
Takriban
watu 24 wamefariki na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali ya treni na
basi ndogo iliyohusisha magari mengine Kusini mwa mji mkuu wa Misri
Cairo.
Treni iligongana na basi ilipokua inatoka mjini Bani Swaif, na
kisha kugonga mahari mengine katika makutano ya njia ya reli umbali wa
kilomita 40 kutoka mji mkuu Cairo.
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zilisema kuwa wengi wa
waliofariki walikuwa jamaa wa familia moja waliokuwa wanarejea kutoka
harusini.
Ajali hiyo ilitokea karibu na kijiji cha Dahshur Jumatatu asubuhi
huku taarifa zikisema kuwa ajali hiyo pia ilihusisha basi ndogo na
magari mengine.
Maafisa wakuu walisema kuwa milango ya magari kuvukia njia ya reli
ilikuwa imefungwa lakini dereva wa treni alishangazwa kuona magari
yakipita kwenye njia hiyo.
Magari ya kuwabeba wagonjwa ya Ambulance, yaliwasili katika eneo la tukio kuwabeba waliojeruhiwa.
Taarifa zinasema kuna hofu kuwa idadi ya waliojeruhiwa huenda ikaongezeka.