October 31 2013 kulikua na mechi ya
Simba vs Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa ambapo timu hizo zilitoka
1-1 huku goli lililoleta malalamiko likiwa ni la Kagera Sugar ambalo
lilifungwa kwa njia ya penat.
Kocha wa Kagera Sugar amesifia maamuzi
ya refa na kusema ‘nafurahi timu imesawazisha kwenye dakika za mwisho na
refa amefanya kazi yake kwa sababu ni siku nyingi sana marefa hawagawi
penat kama hizo, timu nzuri inacheza mpaka goli’
Kocha Kibaden wa Simba kasema ‘nashukuru
tumemaliza mpira salama na vijana wametoka salama, sijafurahishwa na
jinsi mpira ulivyochezeshwa, sitaki kusema hayo kwa sababu watu wana
macho na wanaweza kukosoa lakini uamuzi haukuwa sawasawa, kama
tutaendelea na mpira wa aina hii nafikiri tutaondoka kwenye mwelekeo…
naomba TFF mpya iliyokuja ijaribu
kutazama watu wapumbavu wa aina hii wanaokuja pale kuwaudhi watu,
sijafurahishwa na mpira ulivyochezeshwa mwanzo hadi mwisho na nilijua
kitatokea nini’
