Dereva wa pikipiki ya
abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani
hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa
kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la daraja
la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi
wetu aliyeweza kuwahi kufika ktk eneo la tukio na kutoa msaada wa gari
kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea
Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani,
imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki' daladala iliyokuwa mbele
yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa
uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na
wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya
Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.