Search in This Blog

KINARA WA BANGI TANZANIA NI MKOA WA ARUSHA


IMEBAINIKA kuwa Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi.

Akizungumzia ishu hiyo wakati wa uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Arumeru jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikemea vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku akisisitiza kula sahani moja na wahusika.

Kamanda huyo aliwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara moja wanapogundua uhalifu wa aina hiyo na mwingine wowote.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger