Search in This Blog

"MADADA WA BONGO MUVI WANAHONGWA NA MAWAUME WENYE HELA ZAO NDIO MAANA WANAISHI MAISHA YA JUU".......STEVE NYERERE

Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania (Bongo Movie) Steve Nyerere amesema maisha ya kifahari wanayoonesha wasanii wengi wa kike wa filamu sio maisha halisi yanayotokana na kazi ya filamu wanayofanya.
Akiongea kwenye kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times fm, Steve amesema watu wasiangalie maisha ya kifahari yanayooneshwa na baadhi ya wasanii kwenye magazeti wakadhani kuwa yanatokana na kipato cha filamu wanazofanya.
“Sisi wanaume upande wa Bongo Movie kupata hela tunategemea movies zetu, dada zetu wanahongwa pesa ambapo sisi wanaume hatuwezi ku
hongwa.” Alisema Steve Nyerere.

“Watakuja tu watu wametoka Mererani, wametoka Buzwagi, watakuja watu wametoka wapi kule…wanamtaka dada fulani, kwanza hawawezi kuja pale wakasema 10 hii hapa…dada zetu ni watu wa show shine unawajua tena lazima waoshe. Anunue cheni atoe kwenye gazeti, anunue nini..sasa wanavyoona kwenye magazeti wanadhani hawa watu ndivyo wanavyoishi, wakati sio hivyo," amefunguka.
Msanii huyo ambaye ni moja kati ya wachekeshaji wakubwa nchini aliwalinganisha wasanii wa kike na wasanii wa kiume kwa kuwataja majina kama mfano.
“Leo huwezi kumfananisha JB na Wolper au na Wema, huwezi kumfanisha Steve Nyerere na Shilole, huwezi kuwafananisha hao watu. Kwa sababu yeye ana njia nyingi, kwa sababu yeye kwa siku anaweza akapigiwa simu 34, mimi kwa siku nikapigiwa simu moja tu na producer.”
Muigizaji huyo ambaye pia ni kiongozi katika Bongo Movie Club amewaomba viongozi wa serikali kutoangalia pesa vitu vya kifahari ambavyo zinaandikwa kwenye magazeti na au vinavyonunuliwa na wasanii wa filamu na kuwaza kuwa kuna pesa nyingi imekumbatiwa kwenye tasnia hiyo, na kwamba hali halisi haiko hivyo.
Ameongeza kuwa wasanii bado wanaibiwa sana kazi zao na wanaofaidika zaidi ni watu wanaoiba kazi zao, hivyo serikali iwaangalie kabla ya kuwaza kupata pesa kutoka kwao.
Steve amesema anajipanga kufanya filamu ya 'Good Bye Mr. President', inayohusu Rais Jakaya kuwaaga watanzania.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger