Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova.
.Mtuhumiwa huyo ni wa kumi kukamatwa kuhusiana na tukio hilo
Siku moja baada ya nguli ya sheria za
katiba nchini, Dakta Sengodo Mvungi kuaga dunia nchini Afrika Kusini,
Jeshi la Polis Kanda Maalum Ds, linamshikilia mtuhumiwa mmoja John
Ikondia Mayunga (56) kwa kosa la kushiriki kikamilifu kwenye mauaji ya
mwanasheria huyo na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa
Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa
kiwalani walipata taarifa kwa raia wema kwamba alishiriki kikamilifu
kwenye tukio hilo lilosababisha kifo cha Dakta Sengodo Elibariki Mvungi.
“mnamo tarehe 12/11/2013 Polisi walipata
taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba kuna mtu ambaye amehusika na tukio
la mauaji ya Dakta Mvungi na kwamba kipindi hicho mnamo saa 12 jioni
mtuhumiwa alikuwa maeneo ya mtaa wa Twiga Jangwani akiwa anaangalia
Televisheni,” amesema Kamishina Kova.
1454628_650916231627891_1324435004_n
Marehemu Dakta. Sengodo Mvungi.
Kova amesema kwamba mtuhumiwa
alitambuliwa na kukamatwa kisha kuhojiwa na Polisi na alikubali kwamba
alihusika na akwaongoza Askari hadi nyumbani kwake Kiwalani Migombani.
Alifafanua kwamba taratibu za upekuzi
zilifanyika na katika upekuzi vilipatikana silaha ambayo ni Bastola aina
ya REVOLVER N0. BDN 6111 pamoja na risasi ishirini na moja.
Kova amesema kuwa mtuhumiwa alikiri
kwamba katika vitu vitu vilivyoibwa nyumbani kwa Dakta Mvungi ni pamoja
na bastola hiyo aidha siku ya tukio hilo walitumia milipuko kutishia ili
kufanikisha uporaji huo.
Kamanda Kova alisisitiza kwamba
mtuhumiwa huyo ni wa kumi kukamatwa kuhusiana na tukio hilo na bado
operesheni kali inaendelea ili kuhakikisha kuwa yeyote aliyehusika na
tukio hilo anakamatwa kwa nguvu za dola.
