Search in This Blog

MWANAMKE ATOA TANGAZO LA KUMUUZA MWANAYE KIASI CHA £267 KISA ANAMSUMBUA USIKU HADI ANASHINDWA KULALA


Dunia ina mambo, wakati wengine wanasali usiku na mchana kumwomba Mwenyezi Mungu awawezeshe  kupata japo mtoto mmoja, mzazi huyu wa Brazil yeye ameona isiwe tabu, usumbufu anaoupata usiku kutoka kwa mwanaye suluhisho ni kumuweka sokoni. Mzazi huyo aliweka tangazo la kumuuza mwanaye  kwenye website ya OLX katika  kipengele cha watoto. Katika tangazo hilo mzazi huyo aliandika kuwa anamuuza mtoto kwa £267 ambazo ni sawa na shilingi laki 6 na kitu. Polisi wa Brazil wameanza upelelezi kufuatia tangazo hilo lililowekwa mtandaoni Jumanne katika mtandao wa OLX. Katika tangazo hilo lenye picha ya mtoto huyo mwenye umri wa miezi michache, liliandikwa 'Cries a lot and did not let me sleep and I have to work to survive.' Hata hivyo tangzao hilo lilikaa kwenye mtandao huo kwa zaidi ya masaa 12 tu kabla kampuni hiyo haijaliondoa kwenye mtandao huo kwa kukiuka vigezo na masharti ya kuweka tangazo ambalo ni ‘inappropriate content’
Times Fm
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger